Ijumaa 14 Novemba 2025 - 23:36
Mfadhili wa Israel awaweka waigizaji wanaoiunga mkono Palestina kwenye orodha nyeusi ya Hollywood

Hawza/ Ellison, mmoja wa waanzilishi wa Oracle, mfadhili mkuu wa Israel na muungaji mkono uhalifu wote na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel huko Ghaza, kwa kumteua msimamizi Mwisraeli mwenye misimamo mikali na ukatili mkubwa kwa ajili ya CBC News na kwa kuingilia mali nyingine za Waisraeli katika vyombo vya habari, amewaweka kwenye orodha nyeusi waigizaji ambao walionesha mshikamano na wananchi wa Palestina.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tafsiri cha Shirika la Habari la Hawza, Ellison, mtoto wa Larry Ellison, mmoja wa waanzilishi wa Oracle na mfadhili mkubwa zaidi wa kifedha kwa utawala wa Kizayuni wenye kiu ya damu, baada ya kumbadilisha mkurugenzi wa kituo cha CBC, wale wasanii na waigizaji ambao walionesha kusimama na wananchi wanyonge wa Ghaza na kuyalaani mauaji ya kikatili ya Israel, amewaweka katika orodha nyeusi ya Hollywood na amedai kuwa Israel itawachukulia hatua za kisasi.

Watu hawa waovu wamechukulia hatua yao hii kama moja ya njia za kisasi za Israel dhidi ya barua iliyosainiwa na wasanii mwezi Septemba ya kutaka kususiwa vyombo vya habari vya Kizayuni kutokana na mauaji ya kimbari yanayoendelea Ghaza.

Kwa hakika, orodha hii nyeusi nchini Marekani inaendelea kuongezeka, na kila siku wasanii zaidi wanaunganishwa humo. Marekani ni mahali ambapo kuunga mkono haki za Wapalestina kunazidi kuchanganywa na hotuba za chuki, kwani wanafunzi wa vyuo vikuu wamepoteza ufadhili wao wa masomo kwa sababu ya kusimama na wananchi wanyonge wa Palestina; wanachama wa bodi za ufundishaji wamesimamishwa au kufukuzwa; na mashirika yote ya wanafunzi yamefukuzwa au kutangazwa kuwa yasiyo halali kwa sababu ya kupinga ziara za maafisa wa Israel.

Chanzo: Middle East MONITOR

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha